Mradi wa uhifadhi wa ardhi magharibi mwa Tanzania (LCWT) unafanya kazi ili kulinda idadi ya sokwe walioko hatarini, kulinda makazi yao kupitia mipango ya matumizi bora ya ardhi, kuwezesha jamii za asili kwa kuunga mkono uzalishaji zaidi na maisha endelevu ndani ya mandhari ya Gombe- Masito-Ugalla (GMU). Mandhari ya GMU inapatikana Magharibi mwa Tanzania, inahifadhi zaidi ya 90% ya sokwe wa Tanzania inakadiriwa kama sokwe 2,200.
Idadi hii muhimu ya sokwe inakabiliwa na ongezeko la vitisho kwa sababu ya makazi yao kupotea na mgawanyiko kutokana na ukataji miti haramu, upanuzi wa makazi, na uhifadhi wa makazi kwa ajili ya sababu za kilimo. Sokwe pia moja kwa moja wapo kupata magonjwa kutoka kwenye jamii za karibu za kibinadamu na mgogoro wa binandamu na wanyamapori.
Msingi wa vitishio hivi, ukuaji mkubwa wa idadi wa watu Magharibi mwa Tanzania unaharibu maliasili na kupanua matumizi yasiyoendelevu ya ardhi. Masuala, yakiunganisha na ufanisi duni wa serikali za mitaa kushindwa kusimamia maliasili kwa ufanisi, kumesababisha matokeo pungufu ya uhifadhi.
Ikiongoza na mpango kazi wa uhifadhi wa JGI kwa kiwango cha kitaifa na kikanda, zoezi la Uhifadhi wa Ardhi Mgharibi mwa Tanzania (LCWT) utaongeza ufikiaji wa taasisi kutoka vijiji 74 kwenda vijiji 104 katika wilaya ya mikoa ya Kigoma na Uvinza. Hii inajumuisha makazi ya zamani ya wakimbizi ndani ya Katumba na Mishamo.
Tagi: Mradi wa Pili