Kutafuta namna ya kutokomeza vitisho juu ya uhai wa sokwe na nyani wengine wakubwa kutabaki katika moyo wa utume wa taasisi wa Jane Goodall. Tunafanya kazi kurejesha afya ya makazi kupitia uhifadhi unaozingatia jamii, ili kufikia suluhisho endelevu ambapo watu, sokwe na makazi yako wanastawi pamoja.
Lakini afya ya makazi pekeyake haitoshi. Usafirishaji haramu wa wanyama pori na nyama haramu ya porini na biashara ya kigeni ya wanyama wa majumbani kunapungza idadi ya sokwe ndani ya Afrika. Ili kuelezea hatari hizi, JGI imepitisha mkakati mahiri tunaita “Mbinu ya Pempetatu.” Mbinu ya pempetatu inategemea ushirikiano wa vyombo vitatu tofauti: utekelezaji wa sheria, miradi ya elimu juu ya mazingira, na hifadhi ya wanyama.
Pembetatu: Elimisha. Linda. Okoa
Miradi ya elimu za JGI inahamasisha jamii lengwa, zinafundisha wanajamii kuhusu nini wanaweza kufanya ili kusaidia kulinda nyani wakubwa, na kitakachowakuta wale watakaojaribu kuwadhuru nyani hao. Miradi hii inawezesha watu waweze kutambua pale ambapo kosa linalohusiana na nyani wakubwa limefanyika, na pia mradi unatoa vifaa vya kutolea ripoti kwa mamlaka husika.
Mara baada ya wasimamizi wa sheria umepokea taarifa kutoa kwa raia husika, watakuwa na uwezo wa kuchukuwa hatua stahiki ili kukabiliana na hali ilivyo. Hii mara nyingi inalazimu uzuiaji wa sokwe au nyani mkubwa yeyote. Mara baada ya uzuiaji umetokea, mtuhumiwa atakuwa hatarini mpaka pale wasimamizi wa sheria watakampeleka sehemu salama.