Tunatumia vumbuzi za kisayansi na teknolojia za hivi karibuni katika kutatua changamoto ngumu za uhifadhi. Maarifa haya na vifaa hivi vinatuwezesha sisi kufuatilia afya ya makazi, mgao wa kiramani wa sokwe na nyani wengine wakubwa, na kutazama na kuchambua athari za kibinadamu kwenye makazi muhimu ili kutoa taarifa juu ya hatua za uhifadhi na maamuzi ya usimamizi.
Ilianza na Sayansi, na Sayansi bado inaongoza Njia Yetu
Ilianzishwa na mmoja kati ya wanasayansi mashuhuri, sayansi imekuwa ni msingi wa kazi za Taasisi ya Jane Goodall. Utafiti mkali juu ya sokwe wa Dk Jane Goodall unaendelea kuwa msingi wa mazingatio kwa JGI. Maono yetu ya Uhifadhi wa kisayansi ni kuchunguza, kuvumbua, na kugundua suluhisho mpya, teknolojia na vifaa vya kulinda mazingira na wanyama pori- hususani sokwe, na nyani wengine wakubwa, na makazi yao. Tunakuza uwelewa wetu na ufuatiliaji kwa mizani ya umbali zaidi wa sokwe, makazi na vitisho vinavyotoka kwa binadamu kwenda kwa sokwe barani Afrika, kwa lengo la kuimarisha maamuzi ya uhifadhi.na kukuza ufanisi wa mbinu za uhifadhi kwa kutumia Viwango vy wazi kwa vitendo ili kutunza bioanwai na kupima mafanikio yanayoonekana ya uhifadhi.
Tunaongeza kasi ya kuzifikia data zetu, kwa kuongezea na utafiti wetu wa kuvutia na wa kipekee wa muda mrefu pale Gombe na maeneo mengine ya uhifadhi ndani ya Afrika, kama mali ya kimataifa kwa taaluma mbalimbali za tafiti za kisayansi. Kwa kutambu, kukuza na kusimamia washirika muhimu ili kuvumbua, tuna uwezo wa kuunda suluhisho la ufanisi juu ya changamoto za hifadhi zinazoibuka. Ili kufanya hivi, JGI inatekeleza mbinu za ubunifu kwa kutumia mbinu ya teknologia ya kuhusisha data kulinganisha na sehemu husika, ukijumuisha setilaiti na ndege isiyo na rubani (UAV), simu, kompyuta, utoaji huduma kwa njia ya mtanda, na pia vifaa vya ramani vya tofuti na majukaaa. Pia JGI inazingatia sana sayansi ya wananchi na umati wa watu kwa lengo la kujihusisha na kuwezesha jamii za asili, wafanyamaamuzi, kuwa wasisimamizi bora zaidi wa mazingira, kulinda sokwe na nyani wengine na viumbe hai wote.
Mtazamo wa 360 juu ya Uhifadhi wenye Kutia Uhai Uvumbuzi
Kwa kujenga juu ya msingi wa tafiti za Dk Jane Goodall, JGI inatumia sayansi na teknolojia zilizoendelea katika kuhifadhi aina ya viumbe na makazi yao. Kwa kutumia maarifa haya na vifaa vya hivi karibuni ili kuwezesha jamii za asili, asasi za kiserikali na mashirika yasiyo ya serikali (NGO) ili waweke vipaumbele vyao, JGI, kwa kushirikiana na makundi haya, ili kuweza kuunda na kutekeleza hatua za uhifadhi kwa vitendo ambayo vitaongeza viwango na kasi ya matokeo yetu. Maendeleo ya hivi karibuni juu ya utumiaji wa ndege isiyo na rubani na utoaji taarifa kwa njia ya mtandao kumetuwezesha sisi kutumia picha za setilaiti ili kutoa muhtasari wa kina juu ya makazi wa sokwe wote in Afrika, huku tukitoa kila aina ya azimio linalohitakika katika kutaarifu juu maamuzi mahususi za hifadhi za asili.
Kwa kushirikisha maendeleo haya na washika dau wa ndani, JGI inawezesha jamii, serikali za wilaya na washirika wengine waweze kupata / kufikiwa na taarifa ambazo zilikuwa hazijulikani ambazo zinawawezesha wao katika kutambua vipaumbele vyao na kufafuta suluhisho lenye matokeo chanya juu ya watu, wanyama, na mazingira. Kwa kuleta teknolojia mpya na taarifa zitokanazo na watu wengi ndani ya shughuli za msingi za jitihada za uhifadhi, mbadala wake tunapewa maarifa mapya ya asili, mahitaji na maadili ya wenyeji abayo yanatusaidia sisi kutoa taarifa na kutekeleza kwa ufanisi mikakati ya uhifadhi.