Wenye Ndoto ya Kesho wanachukua Hatua
Mnamo 1991, kundi la vijana wa Kitanzania walikutana na Dk Jane Goodall kwenye ukumbi wake jijini Dar es Salaam, Tanzania, wakiwa na hamu ya kujadili matatizo mbalimbali ambayo wameyashuhudia kwenye jamii zao. Dk Jane Goodall alivutiwa sana na huruma yao, nguvu zao, na shauku yako ya kutafuta suluhisho juu ya matatizo, na ilikuwa kwa sababu ya vijana hawa ndipo ikazaliwa Roots & Shoots.
Toots & Shoots, taasisi ya Jane Goodall ya vijana iliongoza mpango wa hatua za jamii wa kimataifa, ambao unasaidia vijana kuwa raia wa kizazi hiki wenye taarifa na huruma ambao dunia inawahitaji. Tunashirikiana na shule, watoa elimu na mashirika ya vijana ili kuhamasisha na kuelimisha vijana ili waweze kuleta utofauti baina katika ngazi ya kibinaamu.
Vijana Ambao Wanaleta Utofauti Wanaongoza Hrakati kwa Wema.
Kuwezesha vijana ili wajali dunia ambayo wanairithi ni jukumu la kila kizazi. Kupitia mradi wa Roots &Shoots, tunaongoza harakati za kitaifa juu ya hifadhi kwa kuwapa vifaa kizazi chote cha vijana ili wawe raia mashughuli na wenye nia na hamasa kwenye maisha yao ya kila siku. Roots & Shoots inaongezeka kusiko na kifani na kwa kasi katika uhifadhi na mafunzo yanayozingatia misingi ya huduma, ikitoa maarifa na vijana wawe wanajiamini katika kupigania kile wanachokiamini na kuileta utofauti kwa kuwa sehemu ya kitu kikubwa kuliko wanavyojiona.