TAFITI

Uvumbuzi Unafungua Dunia Mpya ya Maarifa na Matumaini

Tangu alivyoweka mguu ndani ya hifadhi ya Gombe, Tanzania mnamo 1960, Dk Jane Goodall ameipa dunia dirisha lisilo la kawaida ndani ya maisha ya ndugu zetu wa karibu. Uvumbuzi wake pale Gombe ultikisa ulimwengu wa kisayansi, na ukafanya sisi tujiulize juu ya mawazo yetu juu ya sokwe, lakini pia hata ubinadamu.

Ilianzishwa mnamo 1965, leo hii Mkondo na Kituo cha Gombe ndiyo makao ya tafiti za muda mrefu zaidi juu ya sokwe na inabaki kuwa kituo cha utafiti za kimaifa ambacho kinatumia mbinu bora zaidi zinazopatikana katika kuendeleza ubunifu wa kisayansi, na kuunga mkono uhifadhi, kuwapa mafunzo wanasayansi wa Kitanzania, na kuendeleza zaidi utafiti wa nyani wa mda mrefu na kufanya uchunguzi ulioanzwa na Dk Jane Goodall. Utafiti huu umeonekana kuwa muhimu juu ya uelewa wetu juu ya nyani na ule wa watu wa kale, na pia tabia ya kisasa ya kibinadamu na afya.

Kuendeleza urithi wa tafiti za Gombe ni muhimu kwa ajili ya uelewa wetu juu ya sokwe, mahitaji ya uhifadhi wake na ufanisi wa mikakati yetu ya kuwaokoa.