Kujenga Kujali Kupitia Ufahamu na Uelewa.
Kupotea kwa makazi na uwindaji haramu kwa ajili ya nyama pori na biashara ya kigeni ya mnyama wa nyumbani ni baadhi ya hatari kubwa wanazokumbana na sokwe. Tunasaidia jamii kuelewa na kufuata sheria ili kulinda aina hii ya viumbe.
Kama taasisi ya Jane Goodall inahitaji kutimiza matokeo ya kweli na ya muda mrefu kutokana na juhudi zetu za kuokoa sokwe wasipotee, ni muhimu kuongeza ufahamu na uelewa juu ya nyani wakubwa kwenye jamii kuhusu aina tofauti za sokwe.
Kwa kuzindua miradi mbalimbali ya elimu juu ya mazingira, JGI inawafikia maelfu ya watu wanaoishi ndani na karibu na makazi ya sokwe. Miradi hii inajuimuisha kampeni kwa kutumia bango la uhamasishaji kwa umma ambalo linafundisha watu kwamba kuua au usafirishaji haramu wa nyani wakubwa ni kosa kisheria, vipindi vya runinga vinavyohusu misitu na wanyama na uhamisishaji wa jamii. La muhimu zaidi ni mpango wetu wa shule, ambao tunalenga kupandikiza heshima na hisia za uwakili wa mazingira kwa watoto ambao siku moja watakuja kusimama kwa ajili ya nyani wakubwa na misitu ambayo wanaita nyumbani.