JINSIA, AFYA NA UHIFADHI

Kuwapa Wasichana Mamlaka Juu ya Afya Zao na Kujifunza ndiyo Jibu:

Afya ya makazi inahitaji jamii zenye afya, na siri ya kufanya jamii ziwe na afya ni kuwawezesha wanawake na wasichana. Wasichana wanaoishi kwenye jamii zilizolengwa na taasisi ya Jane Goodall mara nyingi wanazuiliwa kumaliza elimu, kama wakianza kupata elimu. Hili ni tatizo ambalo haliwaathiri wasichana tu lakini pia jamii zao, familia zao za badae na mazingira yanayowazunguka.

JGI inajua kwamba ili kuwawezesha wasichana wawe na mamlaka na maisha yao ya badae ni kupitia upatikanaji wa elimu kwa kiasi kikubwa na huduma ya afya hakuimarishi tu ustawi wao, lakini pia inapunguza ugandamizaji wa maliasili na inasaidia jamii kustawi. Mpango wa JGI inasaidia wasichana kubaki shuleni kwa kutoa udhamini wa masomo, kutoa taulo za kike, kuunda mtandao wa rika moja wa kusaidiana na kuhakikisha kwamba wasichana wanapata taarifa kuhusu afya zao ili wawe na vifaa vitakavyowafanya waweze kufanya maamuzi muhimu kuhusu uzazi wa mpango na maisha yao.